Kilimanjaro Queens yaenda Nusu Fainali CECAFA Challenge 2016 kwa kuifunga Rwanda 3-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 12, 2016

Kilimanjaro Queens yaenda Nusu Fainali CECAFA Challenge 2016 kwa kuifunga Rwanda 3-2.

Timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imefuzu Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge 2016 kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Rwanda leo,September 12,2016 mjini Jinja, nchini Uganda.

 Kwa kuwa Kundi B lina timu tatu, nyingine ni  Ethiopia.

Ushindi  huo unaihakikishia Kilimanjaro Queens tiketi ya Nusu Fainali.
Mabao ya Kilimanjaro Queens inayofundishwa na Sebastian Nkoma, yamefungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya Rwanda yamefungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.

Kilimanjaro  Queens watashuka tena dimbani kumenyana na Ethiopia Septemba 16, mwaka huu katika mchezo wa mwisho wa kundi lake.

Rwanda na Ethiopia zitakamilisha mechi za Kundi B kwa kumenyanaa na Septemba 14.

Nusu Fainali zitafuatia Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

RATIBA .

Kenya au Harambee Starlets watacheza na  Burundi huku Uganda dhidi ya  Zanzibar ikiwa ni mechi za kundi  “A”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad