Tazama Taswira Picha Kagera Sugar wakijifua Dimba la Kaitaba Bukoba kwa Mara ya Kwanza Agosti 29, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 30, 2016

Tazama Taswira Picha Kagera Sugar wakijifua Dimba la Kaitaba Bukoba kwa Mara ya Kwanza Agosti 29, 2016.


Wachezaji wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba/Bukoba kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni. 

Sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom 2016/2017 ambapo Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 03 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga ambapo mchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya Fifa. 
‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wakiwemo makipa. 

Kurejea katika uwanja wao wa nyumbani Kaitaba kutawahakikishia hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad