Waziri Nape Azifungia Radio 5 na Magic FM Kwa Uchochezi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 30, 2016

Waziri Nape Azifungia Radio 5 na Magic FM Kwa Uchochezi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, ametangaza kuvifungia vituo vya Radio 5 Arusha na Magic Fm Dar kwa muda usiojulikana kwa kosa la uchochezi sambamba n kuielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuvisikiliza kwa kina kisha kumshauri juu ya hatua zaidi za kuchukua.

“Sisi kama Serikali tunatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani, umoja, mshikamano kwa kuwa ni muhimu sana. Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo Agosti 29, 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake Amesema Waziri Nape.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad