Leo(jana,Agosti 18,2016)
nimeamua kuchukua uamuzi wa kutoa agizo kali kabisa toka nimeteuliwa.
Najua
litazua maswali, lakini Kwa kuwa litaokoa maisha ya wanawake wajawazito wa nchi
yetu (CEmOC) na wananchi wengine, nimelitoa. Nitalitetea. Nitalisimamia!
Nimeagiza
ma-DED na ma-DMO wote nchini kuhakikisha wana theatres ZENYE KUFANYA KAZI
IPASAVYO kwenye vituo vyote vya Afya kwenye maeneo yao.
Wiki iliyopita
nilitembelea Manispaa ya Ilala, kwenye vituo vya afya vitatu nilivyotembelea
hakukuwa na theatre yenye kufanya kazi.
Kwa mujibu
wa sera ya afya ya Tanzania, 'kituo cha afya' kitakuwa na hadhi hiyo kama kina
uwezo wa kufanya upasuaji.
Vinginevyo hiyo ni zahanati. Mara nyingi watendaji
hawa wamekuwa wakijificha kwenye kichaka cha 'hatuna fedha', wengine wakiomba
fedha kutoka serikali kuu.
Nilimuuliza
Mkurugenzi wa Ilala, unakusanya sh ngapi Kwa mwezi, akasema bilioni 6.
Nikamuuliza unadhani ni sh ngapi kuwa na theatre yenye kufanya kazi? Akakosa
jibu. Nikampa miezi 6 awe na theatre zenye kufanya upasuaji.
Leo(jana)
nimefanya ziara yangu mikoa ya Shinyanga na Simiyu, nikitimiza mikoa 24.
Huku
pia nimekutana na tatizo hilo hilo nilipokuwa Kishapu, Shinyanga na Mwanhuzi,
Simiyu. Hawa wa Meatu wenyewe wana kituo cha Afya Mwandoya, takriban Km 60
kutoka Hospitali ya Wilaya ya Meatu, pale Mwanhuzi. Wamekipa uwezo wa kufanya
upasuaji.
Wamenunua vifaa, wameajiri hadi Daktari (MD) kwa ajira ya muda kwa
ajili ya kufanya kazi pale.
Kituo
kimefanya takriban operation 40, zote salama Kwa asilimia 100. Wamepunguza msongamano
Mwanhuzi na wamepeleka huduma nyeti na za kuokoa maisha Karibu zaidi na
wananchi, ukizingatia huku hakuna barabara za lami na hakuna ambulances. I was
impressed.
Nikasema
sababu za kuwa Halmashauri hazina pesa huku zinakusanya mamilioni ambayo wanayatumia
bila ku-address matatizo ya msingi ya wananchi hazikubaliki.
Leo iwe mwisho.
Nimeagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini washirikiane na maDMO wajue
watakavyofanya wahakikishe wanafungua huduma za upasuaji kwenye vituo vyote vya
afya nchini ndani ya miezi sita (6).
Baada ya
miezi hiyo sita mimi mwenyewe na timu yangu ya kurugenzi ya ukaguzi na uhakiki
ubora wa huduma za afya (inspectorate and quality assurance) tutasambaa nchi
nzima kukagua huduma hizi na pale ambapo hatutozikuta tutakishusha hadhi kituo
hicho kutoka ngazi ya 'kituo cha afya' na kuwa ngazi ya 'zahanati' sambamba na
kuwashauri wenzetu wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuwa wakuu hao wa idara
wameshindwa kutekeleza majukumu yao na hivyo wawashushe vyeo.
Nitasimamia
uamuzi huu Kwa nguvu zangu zote. Sababu ni kwamba ninajua faida yake. Ninajua
Mungu atafurahi, atanibariki.
Wakati wa
Bunge la bajeti wanaharakati wa haki za wanawake na Watoto waliwahamasisha
Wabunge watushughulikie Kwa ajili ya suala hili. Wakawa-pump wabunge data kuwa
kwa siku magnitude ya vifo vinavyotokana na sababu za uzazi ni sawa na
'coaster' moja ipate ajali na iue watu wote! Wabunge waligeuka mbogo.
Japokuwa
namba hizi zilikuwa exaggerated (zilizidishwa), walifikisha point kwetu. Kwamba
lazima tufanye kitu tofauti kwenye eneo hili. Mimi naanza kuchukua hatua. Vifo
vitokanavyo na uzazi havikubaliki!
Dkt.
Hamisi Kigwangalla, MB., NW-AMJW.
August
18th, 2016.
|
No comments:
Post a Comment