TAZAMA PICHA 4:-Mazingira ya Kufundishia shule ya msingi Kabasharo Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 22, 2016

TAZAMA PICHA 4:-Mazingira ya Kufundishia shule ya msingi Kabasharo Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Mwalimu wa darasa la awali katika shule ya msingi Kabasharo iliyoko kijiji cha Kyota kata ya Kimwani wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Papias Raulian Anthony akifundisha wanafunzi hao wanaosomea chini ya miti wakisumbuliwa na jua huku akitumia ubao (Ceiling board) ukiwa umechanika vipande vipande.

Anthony amesema walimu wako saba wanaofundisha shule nzima na changamoto inawakabili wakati wa kipindi cha mvua ambapo husitisha masomo kutokana na kukosa usikivu wanapolundikana kwenye vyumba vilivyopo na huwa ni kelele na kukosekana njia mbala ya ufundishaji


Amesema katika shule hiyo wananchi walikubaliana na viongozi waliowachagua Kuanzisha darasa moja, kuongeza kuwa matatu lakini kila aliyekusanya michango ya ujenzi hakuiwasilisha na chumba hicho kimekaa miaka saba bila kukamilika ambapo sasa ndipo kimeanza kuendelezwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Kyota.

“Mahitaji mengine kwa wanafunzi hawa ni uhaba wa matundu ya vyoo hakuna choo cha kisasa wanatumia vyoo vya muda matundu mawili yamelazwa mabanzi kwa kuzungushiwa nyasi”Alisema Anthony.

Picha zote kwa hisani ya Shaban Ndyamukama-Muleba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad