TASWIRA PICHA/HABARI:-Magufuli aahidi kuboresha maslahi ya watumishi CCM. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 28, 2016

TASWIRA PICHA/HABARI:-Magufuli aahidi kuboresha maslahi ya watumishi CCM.

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wafanyakazi wa  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma Jana July 27,2016.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho.

Magufuli pia amekutana na  wafanyakazi wa CCM Makao Makuu katika Ofisi za Chama hicho Mjini Dodoma ikiwa ni siku tano tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Tano wa Chama hicho.

Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na watendaji hao wa CCM kwa lengo la kuwasalimia, kupokea maoni na ushauri wao juu ya utendaji kazi ndani ya Chama.

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wafanyakazi wa  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapongeza watendaji wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya na kwa namna ya pekee kwa jinsi walivyotoa mchango mkubwa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la kuendelea kukiimarisha Chama hicho ambacho kimebeba dhamana ya kuongoza Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Dkt. Magufuli amewahakikishia kuwa chini ya uongozi wake atafanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa CCM ikiwemo maslahi duni, vitendea kazi na kuondoa utegemezi.
Aidha, Dkt. Magufuli amewataka watumishi wa chama kutoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki wa mali za Chama litakalosimamiwa na sekretarieti ya chama na ameahidi kuwa atahakikisha mapato yatokanayo na vyanzo vya mapato vya chama yanatumika ipasavyo.

Kwa upande wao watumishi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahaman Kinana wamempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 Mjini Dodoma kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.

Watumishi hao wamemuahidi kuendeleza utumishi uliotukuka na wameelezea matumaini yao ya kuboreshewa maslahi.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akisikiliza maoni na changamoto toka kwa wafanyakazi wa  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma Jana July 27, 2016.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kupata picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma July 27, 2016.
 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad