TASWIRA PICHA BEIJING CHINA:- Mvua yaua Watu 200 huku Milioni 16 wakosa Makazi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 26, 2016

TASWIRA PICHA BEIJING CHINA:- Mvua yaua Watu 200 huku Milioni 16 wakosa Makazi.


Mvua kubwa isiyo ya kawaida imeendelea kunyesha katika Jiji la Beijing China na kusababisha mafuriko ambayo yameuwa watu zaidi ya 200 na wengine mamia hawajulikani walipo huku nyumba zaidi ya 68,000 zikibomolewa na kusababisha zaidi ya watu milioni 16 kupoteza makazi yao.

Picha nyingi zilizopigwa zinonesha mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia  Jumatatu Julai 25, imeathiri zaidi maeneo ya Jimbo la Shaanxi lililopo katika Mji wa  Xi’an, Kaskazini mwa China.

MVUA CHINA (2)
Picha zinaonesha maji kujaa kwenye makazi ya watu huku mali zao zikiwa zinaelea yakiwemo magari na wengine wakibebana ili kuvuka kutoka eneo moja kwenda jingine.

Mvua hizo zilianza kunyesha tangu Jumatatu iliyopita na imesababisha maafa makubwa sambamba na kuahirishwa kwa mechi ya mahasimu wawili wa Jiji la Manchester Uingereza, Manchester United na Manchester City kutokana na uwanja kujaa maji. Mechi ilitarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia Jana Jumatatu.
MVUA CHINA (1) MVUA CHINA (3) MVUA CHINA (4) MVUA CHINA (5) MVUA CHINA (6) MVUA CHINA (7) MVUA CHINA (8) MVUA CHINA (9) CHINAS CHINASSSIn this Thursday, July 21, 2016, photo, rescuers use a raft to transport people along a flooded street in Shenyang in northeastern China's Liaoning Province. Dozens of people have been killed and dozens more are missing across China after a round of torrential rains swept through the country earlier this week, flooding streams, triggering landslides and destroying houses. (Chinatopix Via AP)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad