Kitambi ni hali ya kiafya ya mtu
mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa kiasi
kikubwa.
Mtu akiwa na kitambi anapata athari
kubwa ikiwamo kupungua kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo
kubwa la kiafya duniani.
Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.
Katika mawazo ya kizamani na hata sasa katika
baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni tajiri.
Tatizo la unene na vitambi litazidi
kuongezeka ikiwa serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za
dharura na mipango madhubuti kulikabili.
Vitambi hupunguza maisha ya watu
wenye hali hiyo ya afya, hivyo kusababisha upotevu wa rasilimali watu.
Ili kuepukana na athari hiyo watu
wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi na milo yao.
Wengi wana muda mchache
sana wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo
wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na
vitambi.
Kuna wengi wanatambua athari za
tatizo la unene na vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii
inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na
afya njema.
Watu wengi, hasa vijana wamekuzwa kwa kula
chipsi, mikate na vyakula vya sukari na si mbogamboga na matunda.
Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi
mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi
wanaongezeka kila sehemu.
Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye
kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la
kawaida.
MAGONJWA
Hii inatokana na ukweli kwamba uzito
wa mtu husababisha magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo
huua mamilioni ya watu duniani kote.
Kifupi ni kuwa ukiwa na mafuta mengi mno
utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya kupanda kwa presha, magonjwa
ya moyo, kansa.
Kuongeza uzito au
kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi
mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili,
kuuzunguka moyo na ndipo matatizo yanapoanza.
USHAURI
Kila mtu aepuke kula vyakula vyenye
mafuta mengi na kutokula chakula kupindukia na ule unaposikia njaa, kutotia
mafuta mengi kwenye chakula na kutotumia sukari nyingi.
Kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya
kukimbia, kutembea au kuogelea angalau kwa nusu saa kila siku.
Watu wanashauriwa kuacha kutumia
vyakula vya kopo na hasa vile vyenye gesi nyingi. Wale ambao ni wanene kupita
kiasi waonane na daktari kwa ushauri wa kitaalamu.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
|
Tuesday, July 26, 2016
AFYA YAKO:-Athari ya kitambi kiafya.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment