Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka
wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha
mikopo yao.
Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka
waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi
cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda
kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza
kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha
mikopo yao.
Zoezi hili litajumuisha pia waajiri
ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.
Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote
watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha
sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo basi, wanufaika wa mikopo
wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za
waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni
yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika.
Marejesho yanaweza
kufanyika kupitia Akaunti:-
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili
kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu.
|
No comments:
Post a Comment