EURO 2016 -MATOKEO / RATIBA ROBO FAINALI:- Ureno na Nusu Fainali bila kushinda katika Dakika 90. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 01, 2016

EURO 2016 -MATOKEO / RATIBA ROBO FAINALI:- Ureno na Nusu Fainali bila kushinda katika Dakika 90.

Wachezaji wa Ureno Pepe, Ronaldo na mwenzao wakishangilia baada ya  Ricardo Quaresma kufunga penati ya mwisho na kuiwezesha timu hiyo kushinda kwa penalti 5-3 mchezo wa Robo Fainali ya Euro 2016 dhidi ya Poland usiku wa Jana June 30, 2016 kwenye Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille, Ufaransa. 

Kwa matokeo hayo,Ureno imetinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa na kuwa nchi ya kwanza kufuzu katika hatua hiyo baada ya kuwafunga Poland kwa mikwaju ya penalti 5-3.

Dakika 120 zilishuhudia mchezo huo ukiisha kwa suluhu ya goli 1-1.
Pichani Ricardo Quaresma alikuwa shujaa kwa timu yake baada ya kupiga penati ya mwisho iliyoivusha katika hatua nyingine huku kiungo wa Jakub Blaszczykowski akikosa mkwaju wa penati kwa upande wa Poland.

Robert Lewandowski alitangulia kuifungia Poland dakika  ya 12 ya mchezo, kabla ya Renato Sanches kuisawazishia Ureno dakika ya 33.

Ureno itakutana katika hatua ya nusu fainali July 06, 2016 na mshindi wa mchezo kati ya Wales na Ubelgiji unaochezwa leo July 1, 2016, saa nne usiku.
Ureno walifunga Penati zao zote 5 zilizopigwa na Ronaldo, Renato Sanchez, Joao Moutinho, Nani na Ricardo Quaresma.

Wapigaji wa Poland waliopiga Penati na kufunga ni Lewandowski, Arkadiusz Milik, Kamil Glik na Jakub Blaszczykowski kukosa Penati yake iliyookolewa na Kipa Rui Patricio na kuifanya Ureno ishinde Penati 5-3.

DONDOO MUHIMU.

 -Ureno ni Nchi ya Kwanza kutinga Nusu Fainali ya EURO 2016 bila kushinda hata mchezo 1 katika Dakika 90.

 -Hii ni mara ya 5 kwa Ureno kufika Nusu Fainali za EURO katika ushiriki wao wa 7.
EURO 2016 -MATOKEO / RATIBA ROBO FAINALI.

**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo

Ijumaa Julai 01, 2016.

(Stade Pierre Mauroy, Lille)

Wales v Belgium

Jumamosi Julai 02, 2016.

(Stade de Bordeaux)

Germany v Italy

Jumapili Julai 03, 2016.

(Stade de France, Paris)

France v Iceland

NUSU FAINALI

**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo

Jumatano Julai 06, 2016.

(Stade de Lyon)

Portugal v Wales au Belgium

Alhamisi Julai 07, 2016.

(Stade Velodrome, Marseille)

Germany/Italy v France/Iceland

FAINALI

Jumapili Julai 10, 2016.


**Saa 4 Usiku, Saa za Bongo
(Stade de France, Paris)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad