AJALI / PICHA :-Magari matatu yasababisha vifo Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 01, 2016

AJALI / PICHA :-Magari matatu yasababisha vifo Morogoro.

Habari iliyoripotiwa na ROAD SAFETY AMBASSADORS (RSA)-TANZANIA asubuhi ya leo July 1, 2016, ni kuhusu ajali ambayo imetokea eneo la  DAKAWA mkoani Morogoro ikihusisha magari matatu ambayo ni lori la mafuta, Semi pamoja na Basi.

Taarifa hiyo inasema kuwa Kuna abiria wamekufa ikiwajumuisha na madereva wote wawili na wasaidizi wao pamoja na abiria wengine.

Miili ya marehemu imehifadhiwa  hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa utambuzi huku Majeruhi wanapatiwa matibabu hapo hospitali ya ST JOSEPH inayomiliikiwa na Kanisa la Roman Catholic.
Ajali hiyo iliyotokea Jana June 30, 2016 majira ya saa 9 Usiku baada ya tanker na Semi kugongana na gari hizo kuwaka moto, baadaye kidogo Basi la OTTA lenye namba za Usajili T 201 DGK kutoka Bukoba kuelekea Dar likaigonga mojawapo ya gari zilizopata ajali kama unavyoona kwenye picha.

 Wito, Kama una ndugu unahisi au unafahamu alikuwa anasafiri basi fanya mawasiliano naye mapema. TAARIFA HII KWA HISANI YA ROAD SAFETY AMBASSADORS (RSA)-TANZANIA


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad