Bi.Valerie
Msoka (Kushoto Pichani ) kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), akiongoza
kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka 2016
yanayofanyika kitaifa katika hoteli ya ufukweni ya Malaika Jijini Mwanza.
Kauli mbiu
ya Maadhimisho haya mwaka huu ni 2016.."Kupata Taarifa ni Haki yako ya
Msingi:Idai'".
Maadhimisho haya yanafanyika kitaifa kwa mara ya nne na
yanalenga kukumbusha Umma na dunia kwa ujumla umuhimu wa vyombo vya habari
kufanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu ama chombo chochote.
Zaidi ya
wadau 250 wakihusisha waandishi wa habari wakongwe na wapya, wahariri, viongozi
wa mashirika wahisani (ya kimataifa na ya hapa nchini) wawakilishi wa mihili ya
nchi, wasomi wa vyuo vikuu na balozi mbalimbali wamekusanyika jijini hapa kwa
maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni kesho,May 03, 2016.
Watoa Mada
katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2016
yanayofanyika Jijini Mwanza. Kilele cha Maadhimisho hayo kinafanyika kesho Mei
3,2016 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed
Chande Othman.
Pia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape
Nhaute pamoja na wageni wengine waalikwa wanatarajia kuhudhuria maadhimisho
hayo.
|
No comments:
Post a Comment