VPL 2015/2016:- Kiiza aipa Simba SC ushindi na sasa Wapo Kileleni baada ya Misimu 3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 13, 2016

VPL 2015/2016:- Kiiza aipa Simba SC ushindi na sasa Wapo Kileleni baada ya Misimu 3.

Hamisi Kiiza akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga
Mchezaji wa Simba SC,Hamisi Kiiza akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga,Leo February 13,2016.

Mabao mawili ya Hamisi Kiiza yanaipandisha Simba SC kileleni mwa ligi Kuu Vodacom Tanzania bara 2015/2016 kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa misimu mitatu bila kukaa kileleni mwa ligi kuu  na kuacha ligi hiyo ikitawaliwa na mahasimu wao Yanga SC, Azam FC na Mtibwa Sugar ambao wamekuwa wakipokezana kuongoza ligi hiyo.

Kwa mara ya mwisho Simba SC iliongoza ligi mwanzoni mwa msimu wa 2013 /2014 wakati huo Simba SC ikiwa chini ya kocha Abdalah Kibadeni aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kuiongoza Simba SC kushinda michezo yake mitano ya mwanzo.

Ibrahim Ajib (kushoto) akipambana na beki wa Stand United
Mwinyi Kazimoto (katikati) akisaidiwa kutoka nje na madaktari baada ya kuumia uwanjani
Mwinyi Kazimoto (katikati) akisaidiwa kutoka nje na madaktari baada ya kuumia uwanjani.

Kwa ushindi huo wa Bao 2-1 Simba SC walipocheza na Stand United huko Kambarage Jijini Shinyanga na Simba SC sasa wapo kileleni wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi 19 wakiguatiwa na Yanga SC wenye Pointi 43 kwa Mechi 18 na wa 3 ni Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 16.

Hadi Mapumziko, Simba walikuwa mbele 1-0 na Kipiundi cha Pili Kiiza tena kuwapa Bao la pili na mwishoni Stand United kufunga Bao lao moja.
Hassan Kessy akimwacha kwenye mataa Amri Kiemba
Huko Sokine, Mbeya, Wenyeji Mbeya City waliitwanga Toto Africans Bao 5-1 kwa Bao za Rafael, Ramadhan Chombo, Boban, Bao 2 na Meshak.

Mechi inayofuata kwa Simba SC kwenye VPL ni February 20 ,2016 wataingia kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC wakiwa na morali ya juu baada ya kushinda michezo yao sita kabla ya pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wao huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 2-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.
Baadhi ya viongozi wa Simba wakifatilia mechi ya Stand United vs Simba
Baadhi ya viongozi wa Simba SC wakifatilia mechi ya Stand United vs Simba SC.

Yanga SC ambao wikiendi hii hawana Mechi ya VPL kwa vile Leo walikuwa huko Visiwani Mauritius kucheza Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI walipoipiga Cercle de Joachim 1-0 kwa Bao la Donald Ngoma.

MATOKEO.

Jumamosi Februari 13,2016.

Stand United 1 – 2 Simba SC   

Mgambo JKT 0 – 1 African Sports  

Mbeya City 5 – 1 Toto Africans        

Ndanda FC 1 – 0 Majimaji     

JKT Ruvu 1 – 1 Kagera Sugar 

VPL 2015/2016 -LIGI KUU VODACOM

Jumapili Februari 14,2016.

Mwadui FC v Tanzania Prisons   

Coastal Union v Azam FC 

Jumamosi Februari 20,2016.

Yanga SC v Simba  SC 

Mgambo JKT v Tanzania Prisons 

Stand United v JKT Ruvu  

Mbeya City v Azam FC     

Majimaji v Mtibwa Sugar  

Toto Africans v Kagera Sugar     

Jumapili Februari 21,2016.

Ndanda FC v African Sports       

Mwadui FC v Coastal Union


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad