VPL 2015/2016:- Coastal Union waitandika Azam FC 1 – 0 Leo February 14. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 14, 2016

VPL 2015/2016:- Coastal Union waitandika Azam FC 1 – 0 Leo February 14.

Wachezaji wa Mwadui FC na TZ Prisons wakiwania mpira.

Azam FC imeshindwa kuiengua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC, baada ya jioni ya leo,February 14,2016,kufungwa bao la dakika ya 68 la Miraj Adam na kuwapa Coastal Union ushindi wa Bao 1-0 walipocheza nyumbani  huko Mkwakwani ,Tanga Mechi ya Ligi Kuu Vodacom.

Kipigo hiki ni cha kwanza kwa Azam FC tangu VPL ianze Msimu huu na ni pigo kwao kwani wamekosa nafasi murua ya kushika uongozi wa Ligi.
Kelvin Sabato (kulia) wa Mwadui FC akichuana na , Nurdin Chona (kushoto) wa TP Mazembe.

Simba SC, ambao Jana,February 13,2016, waliipiga Stand United 2-1 huko Kambarage Shinyanga, wanabakia kileleni wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi 19 wakifuatiwa na Yanga SC wenye Pointi 43 kwa Mechi 18 na wa 3 ni Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 17.

Nurdin Chona akitibiwa na madaktari wa TZ Prisons baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Mwadui .

Mechi nyingine ya VPL iliyochezwa Leo ilikuwa huko Shinyanga ambako Mwadu FC na Tanzania Prisons zilitoka 0-0.

VPL 2015/2016-LIGI KUU VODACOM

Ratiba-Jumamosi Februari 20,2016.

Yanga SC v Simba SC      

Mgambo JKT v Tanzania Prisons 

Stand United v JKT Ruvu  

Mbeya City v Azam FC     

Majimaji v Mtibwa Sugar  

Toto Africans v Kagera Sugar     

Jumapili Februari 21,2016.

Ndanda FC v African Sports       

Mwadui FC v Coastal Union


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad