AHADI YETU:-Mbunge wa Jimbo la Lindi CCM atimiza Moja ya Ahadi yake Jimboni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 18, 2016

AHADI YETU:-Mbunge wa Jimbo la Lindi CCM atimiza Moja ya Ahadi yake Jimboni.

Mh Hassani Selemani Kaunje ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Lindi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) leo January 18,2016 , ameweza kutekeleza ahadi yake aliyowaahidi kikundi cha wanawake wachuuzi wa samaki cha Mitwero ya kuwapatia msaada wa Majokofu mawili (2) ya kutunzia Samaki.

Akikabidhi majokofu hayo leo hii Mh. Mbunge amewataka wachuuzi hao kutunza vitu hivyo kwani ni vyagharama na vitadumu kwa muda mrefu endapo wataviweka katika mazingira mazuri. 

Nao wanakikundi hicho cha akinamama wachuuzi wa samaki wameweza kupongeza hatua hiyo, wamemsifia kuwa ni mtu wa kutimiza ahadi kwani ametimiza kile alicho ahidi.
Mh. Mbunge amekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi zake kwa kipindi hiki kifupi tangu alipochaguliwa na wananchi wa jimbo la Lindi mjini kwani hivi karibuni aliweza kutoa msaada wa Matanki ya kutunzia maji katika kata ya Kineng'ene.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad