Naibu Katibu
Mkuu (TAMISEMI) Dk. Deodatus Mtasiwa akitoa ufafanuzi wa jambo kwenye mkutano
huo na wanahabari (hawapo pichani).
|
Kutoka
kushoto ni, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk. Neema Rusibamayila,
Naibu Katibu Mkuu (Tamisemi), Dk. Deodatus Mtasiwa na Kaimu Katibu Mkuu, John
Michael.
|
Wanahabari
wakichukua tukio hilo.
SERIKALI ya
Tanzania kupitia Wizara ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na
Watoto leo imetoa ripoti yake ya wiki juu ya mwenendo wa kipindupindu hapa
nchini.
Akizungumza
na wanahabari leo,January 18,2016, jijini Dar es Salaam katika ofisi za wazara hiyo, Mkurugenzi
wa Huduna za Kinga Nchini, Dk. Neema Rusibamayila amesema kuwa katika kipindi
cha wiki moja kuanzia Januari 11 hadi 17,2016 kulikuwa na wagonjwa wapya 549 na
vifo 10 huku mikoa iliyoripoti kuwa na ugonjwa ikiongezeka kutoka 11 hadi kufikia
16 ukilinganisha na wiki iliyopita.
Rusibamayila
amesema, mikoa hiyo iliyoongezeka kwa kurudia kuripoti wagonjwa wapya baada ya
kudhibiti ugonjwa kwa wiki zilizopita ni Dar es Salaam, Lindi, Rukwa, Kagera na
Kilimanjaro huku akiongeza kuwa bado kuna mikoa inaendelea kuripoti wagonjwa
ikiwa ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani ,Dodoma, Geita,
Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu.
Aidha,
alisema Mkoa wa Morogoro unaendelea kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa (Manispaa
ya Morogoro wagonjwa 120, Halmashauri ya Morogoro wagonjwa 40 ) ikifuatiwa na
Mkoa wa Simiyu wenye idadi ya watu 50.
Hata hivyo,
Rusibamayila ameeleza namna mwananchi anavyoweza kupata huduma ya kufahamu
dalili za ugonjwa huo wa kipindupindu kupitia njia ya simu ya mkononi kwa kupiga
namba 117 kisha kusikiliza ujumbe wa
sauti, au kuandika ujumbe wa maneno “kipindupindu/cholera” kwenda namba
15774 na huduma hiyo haina malipo yoyote
kwa mtumiaji.
Alisema
kuanzia Agosti mwaka jana 2015, ugonjwa huo ulipoanza hapa nchini hadi jana Januari
17, 2016 jumla ya watu 14,105 wameugua
ugomjwa huo na kati yao 218 wamepoteza maisha kwa maradhi hayo ya kipindupindu.
NA DENIS
MTIMA/GPL.
|
No comments:
Post a Comment