Aliyekuwa
nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ leo January 18,2016, amepeleka barua TFF ya
kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Tanzania kutokana kunyang’anywa
unahodha bila utaratibu maalum na kupewa nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana
Samatta.
Cannavaro
amesema, hakukuwa na tatizo kumpa unahodha Mbwana Samatta kwasababu anastahili
kuwa nahodha wa kikosi cha taifa lakini amelalamikia utaratibu uliotumika
kumvua unahodha huo na kumpa Samatta.
Amedai kuwa,
hakupewa taarifa rasmi zaidi ya kuona kwenye TV na vyombo vingine vya habari
kuwa amevuliwa unahodha na kupewa mtu mwingine.
Cannavaro
ameongeza kuwa watangulizi wake Salumu Swed na Shadrack Nsajigwa waliagwa kwa
heshima lakini yeye hajapewa taarifa rasmi hivyo anaona amedharauliwa.
Beki huyo
kisiki wa klabu ya Yanga SC amesema, alikuwa bado anauwezo wa kuitumikia Taifa Stars
kwa miaka mingine minne ijayo lakini ameamua kustaafu kutokana na kudhalilishwa
kwa kuvuliwa unahodha kwenye vyombo vya habari.
“Nilikuwa na
uwezo wa kucheza hata miaka mingine minne inayokuja kulitumikia taifa langu.
Naipenda nchi yangu mimi ni mzalendo halisi, nimelitumikia taifa hili kwa miaka
10 na nilikuwa na nia ya kulitumikia kwa miaka mingine minne mbele lakini
kitendo kilichofanywa cha kunivua unahodha kwenye TV kimenidhalilisha”, amesema
Cannavaro.
“Sikuona
kuthaminiwa, jitihada zangu zote za kujitolea kwa taifa hili hazikuthaminiwa.
Mimi na Samatta ni marafiki, Samatta ni rafikiyangu sana na anastahili kuwa
nahodha wa national team”.
“Kocha
Boniface Mkwasa mimi namkubali sana tangu tukiwa Yanga, ni mtu ambaye
hatujawahi kukwaruzana”.
“Mimi
sijajiuzulu kwa kukasirika kutokana na kuvuliwa unahodha au Mbwana Samatta
kupewa unaodha, kilichoniudhi mimi ni utaratibu uliotumika kunivua unahodha.
Sikutegemea kuona navuliwa unahodha nikiwa nimekaa kwenye TV naangalia mechi ya
Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar ya michuano ya Mapinduzi Cup”.
“Ilitakiwa
kocha anipigie simu anitaarifu tukae chini nipewa taarifa na mimi nikubali.
Salumu Swed alikuwa nahodha wa timu ya taifa alipostaafu tulimuaga Mwanza.
Shadrack Nsajigwa ambaye mimi nimechukua mikoba kwake aliagwa vizuri na kwa
amani kabisa lakini mimi nimedharaulika”.
Siku tatu
baada ya Samatta kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji
wanaocheza ligi za Afrika, kocha mkuu wa Taifa Stars Boniface Mkwasa
alimtangaza rasmi Samatta kuwa ndiye nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania
huku Cannavaro akipewa majukumu ya kuwa nahodha wa kikosi cha taifa
kinachoshiriki CHAN lakini Mkwasa
akasema wanamtafutia nafasi nyingine kwenye kikosi cha Stars.
Mkwasa
alimtangaza Samatta kuwa nahodha Taifa Stars wakati akiwa visiwani Zanzibar
akifatilia michuano ya Mapinduzi Cup 2016 iliyomalizika juma lililopita.
Source:-Shaffihdauda.
|
Monday, January 18, 2016
Home
MICHEZO
BREAKING NEWS:- Nadir Haroub ‘Cannavaro’ astaafu kuchezea timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
BREAKING NEWS:- Nadir Haroub ‘Cannavaro’ astaafu kuchezea timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment