|
Waziri Mkuu wa Tanzania,
Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Eng.
John Ndunguru kukamilisha uchunguzi wake na kumpatia taarifa ya maandishi juu
ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma unaohusisha uuzwaji wa jengo la
KIGODECO na viwanja 12 vya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambao unadaiwa kukiuka
taratibu.
Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumatano, Desemba 30, 2015) kwenye
ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma wakati akizungumza na viongozi na watendaji
mbalimbali wa mkoa huo alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku
mbili mkonai humo.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema anazo taarifa kuwa jengo hilo
liliuzwa kwa sh. milioni 370/- pamoja na jengo jingine la MIBOS kwa sh. milioni
50/- licha ya kupewa barua na Mkuu wa Mkoa huo kusitisha uuzwaji wa jengo
pamoja viwanja hivyo, bado liliuzwa. “Katibu Tawala wa Mkoa kaa na Mkurugenzi
wa Manispaa, Mhandisi wa Manispaa na Mhasibu na unipatie taarifa kwa maandishi
ifikapo Jumamosi hii,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
“Nataka kujua
nani alifanya tathmini ya jengo, ni kwa nini jengo liliuzwa kwa thamani hiyo,
je ndiyo thamani halisi ya jengo? Ni kwa nini RC alipozuia, utaratibu
uliendelea? Je, utaratibu wa uuzaji ulifuatwa? Ni kwa nini viwanja viliuzwa
chini ya thamani,? Katibu Tawala kaa na watu wako na uniletee hiyo taarifa kwa
maandishi.
Tukigundua kuna mianyamianya tutachukua hatua za kinidhamu,”
alisema.
Viongozi walioagizwa kukutana na Katibu Tawala wa Mkoa ni Mkurugenzi
wa Manispaa, Eng. Boniface Nyambele; Mhandisi wa Manispaa, Eng. Boniface William
na Mhasibu wa Mapato wa Manispaa, Ndg. Bawili Mkoko.
Kuhusu uuzwaji wa jengo na
viwanja, imebainika kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Luteni Kanali (Mst), Issa Machibya
alizuia uuzaji huo kwa barua ya tarehe 16 Juni 2015 akitaka viwanja hivyo
vitumike kwa matumizi ya manispaa na mchakato huo usitishwe hadi mwakani lakini
agizo lake lilipuuzwa na jengo likauzwa kwa sh. milioni 370 ambayo ni bei ya
kiwanja pekee.
Tuhuma nyingine zinazopaswa kuchunguzwa ni pamoja na matumizi ya
sh. milioni 809 kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Kiasi hicho
kilitolewa kutoka kwenye fedha za miradi ya maendeleo (Capital Development
Grants-CDG), Mradi wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo (ASDP),
Mradi wa Uendelezaji Miji (Tanzania Strategic Cities Programme –TSCP) na Miradi
ya Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEDP).
Inadaiwa kwamba Mkurugenzi huyo kwa
kushirikiana na baadhi ya watumishi wa idara ya mipango na fedha walitumia
ujenzi wa maabara kama kigezo cha kuchota fedha hizo bila kutoa taarifa kwa
wakuu wa idara husika ambao walikasimiwa fedha hizo.
Tuhuma nyingine ni
manunuzi hewa ya vipuri (spare parts) vyenye thamani ya sh. milioni 8 na
manunuzi hewa ya stationeries yenye thamani ya sh. milioni 4.6/-. Haya
yanadaiwa kufanywa Julai 25, mwaka huu 2015 na Mkurugenzi huyo akishirikiana na
Mhasibu Mkoko.
Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam mchana huu.(mwisho).
IMETOLEWA
NA:-
OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATANO, DESEMBA 30, 2015.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
Thursday, December 31, 2015
Home
HABARI
SIASA
UFISADI KIGOMA:-Waziri Mkuu Atoa siku Mbili Kwa Katibu Tawala wa Mkoa Juu ya tuhuma za uuzwaji wa jengo la KIGODECO na viwanja 12.
UFISADI KIGOMA:-Waziri Mkuu Atoa siku Mbili Kwa Katibu Tawala wa Mkoa Juu ya tuhuma za uuzwaji wa jengo la KIGODECO na viwanja 12.
Tags
# HABARI
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.





No comments:
Post a Comment