TAZAMA PICHA:- Ngoma za Asili zanogesha Uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mafuta ya Alizeti Kahama/Shinyang’a. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 08, 2015

TAZAMA PICHA:- Ngoma za Asili zanogesha Uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mafuta ya Alizeti Kahama/Shinyang’a.

Msanii mwenye fani nyingi maarufu kwa jina la CHAPCHAP akitoa burudani katika viwanja vya CDT mjini Kahama,msanii huyo mwenye makazi yake mkoani Shinyanga huwa anaimba nyimbo za kiutamaduni,dansi,vichekesho na maigizo na mara kwa mara amekuwa akifanya kazi na shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ).

Hapa ni katika viwanja vya CDT vilivyopo mjini Kahama mkoani Shinyanga ambapo leo Jumapili Desemba 06,2015 kumefanyika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mafuta ya alizeti yaliyoongezwa virutubisho vya Vitamini A.Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kahama Michael Mzengula ambaye ni afisa kilimo wa manispaa hiyo.

 Kampeni hiyo imeandaliwa na shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) wakishirikiana na shirika la Menonite Economic Development Association(MEDA) na shirika la Ushauri na Udhibiti wa Ukimwi Kahama (SHIUUKA).

Mradi huu wa mafuta ya asili ya alizeti yenye vitamini A umeanzia katika mikoa ya Manyara na Shinyanga baada ya utafiti kuonesha kuwa mikoa hiyo ina tatizo la upungufu mkubwa wa Vitamini A kwa watoto na akina mama.



Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC) akiwa na mwenzake wakitoa nyoka aina ya Chatu.

.........Hapa..........akicheza na nyoka aina ya Chatu.


Kushoto mwenye nguo nyeusi ni mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) lenye makao makuu yake mkoani Shinyanga Musa Jonas Ngangala akifuatiwa na mkurugenzi wa Malunde1 blog yenye makao yake makuu mkoani Shinyanga Kadama Malunde wakiwa katika picha ya pamoja na Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC)..TAZAMA PICHA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA

Mkazi wa Kahama akiwa amebeba mtoto akifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa uzinduzi huo ambapo miongoni mwa faida za vitamini A ni kusaidia ukuaji bora na maendeleo ya mtoto.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad