KAMPENI YA USAFI KITAIFA:-DC Ngara ahimiza Usafi wa Mazingira na usafi binafsi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 08, 2015

KAMPENI YA USAFI KITAIFA:-DC Ngara ahimiza Usafi wa Mazingira na usafi binafsi.Mkuu wa Wilaya ya Ngara,mkoani Kagera Bi. Honoratha Chitanda akizungumza na Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kabanga,mjini Kabanga jana December 07,2015 wakati wa Kampeni  ya usafi wa mazingira na usafi binafsi iliyoizindua December 05,2015 mjini Ngara ambayo inaendelea wilayani humo na taifa zima kwa ujumla.

Amewahimiza wananchi kufanya Usafi wa mazingira ikiwa ni njia ya kuendeleza afya bora kwa kuzuia mlipuko wa magonjwa unaoletwa na athari za taka.

Pia aliambatana na Viongozi wengine wa wilaya kutembelea kata ya kabanga, eneo la mji mdogo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi .

Mara alipowasili eneo la kabanga alianza na zoezi la kuokota takataka zilizo zagaa akishirikiana na wananchi ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni ya usafi aliyoizindua siku ya Jumamosi ya tarehe 05/12/2015 katika eneo la Kojifa mjini Ngara.

Aidha pia mkuu huyo wa wilaya ya Ngara,Bi.Chitanda mara baada ya zoezi la usafi alifanya Mkutano wa Hadhara ili kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambapo baadhi ya wakazi wa mji wa kabanga wameeleza kero zao mbalimbali zinazo wakabili ikiwemo mgogoro kutumia stendi ya magari ambayo ipo eneo lenye mgogoro wa ardhi.BOFYA HAPA KUSOMA NA KUTAZAMA PICHA ZAIDI.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad