TASWIRA PICHA:-Mtu mmoja auawa,wanne wajeruhiwa wakiwemo Polisi baada ya vurugu za wakulima na wafugaji Mvomero. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 14, 2015

TASWIRA PICHA:-Mtu mmoja auawa,wanne wajeruhiwa wakiwemo Polisi baada ya vurugu za wakulima na wafugaji Mvomero.

Baada ya  Rais wa Tanzania ,Dr John Pombe Magufuli kutangaza Baraza jipya la Mawaziri na wengine tayari wameanza kazi… Waziri Mwigulu Nchemba yeye ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, na leo December 14,2015 Waziri Mwigulu Nchemba amelazimika kusafiri mpaka mkoani Morogoro baada ya kuripotiwa kwa taarifa ya ishu ya mapigano kati ya wakulima na wafugaji, mtu mmoja amefariki, wengine wamejeruhiwa wakiwemo Askari Polisi pia.

Chanzo cha mgogoro huo kimetajwa kuwa ni ishu ya mfugaji mmoja kulalamikiwa kuingiza mifugo kwenye shamba la mkulima mmoja na kutokea ugomvi huo mkubwa kati ya wakulima na wafugaji.
Mapigano hayo ya wakulima na wafugaji yametokea katika kijiji cha Dihinda wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Dihinda kuwa mapigano hayo yaliibuka baada ya mfugaji mmoja wa jamii ya kimasai kudaiwa kuingiza Mifugo kwenye shamba la mazao jamii ya mikunde,la Bwana Bakari Mlunguza ambapo wakulima waliingilia kati na kuwakamata ng'ombe takribani 100 wa mfugaji huyo na kuzipeleka kwenye ofisi ya kijiji.

Ilielezwa zaidi kuwa wakiwa ofisini hapo katika kikao cha pamoja na mmiliki wa mifugo hiyo,viongozi wa kijiji na mkulima ambaye Mazao yake yanadaiwa kuliwa na Mifugo,iliamuriwa mfugaji huyo alipe  shilingi laki mbili kama fidia kwa mazao yaliyoliwa,jambo ambalo aliafiki katika kikao lakini badala yake akataka kuondoka bila kulipa fidia.

Hata hivyo wakulima walipinga kitendo hicho na kuzuia Mifugo hiyo isiondolewe kabla ya fidia,lakini kundi la wafugaji liliingilia kati na kusababisha vurugu ambapo mkulima mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwa kukatwa katwa mapanga ambapo wananchi nao walivamia Mifugo iliyokuwa ikishikiliwa na kuwaua ng'ombe 72.

Wakati tukio hilo likitokea,askari polisi walifika eneo la tukio kudhibiti vurugu zilizo lakini wafugaji waliwajeruhi askari wawili na kufanya jumla ya watu wanne kujeruhiwa katika tukio hilo na kulazwa hospitali ya misheni ya Bwagala iliyopo wilayani Mvomero.

Tayari Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba,kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro na wilaya ya Mvomero wamekwenda eneo la tukio kufahamu zaidi chanzo cha tukio hilo na kuzungumzia na wananchi wa makundi ya wakulima na wafugaji.

Source:-Itv.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .Post Bottom Ad