VPL 2015/2016:-Huu ndio msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara baada ya mechi za December 12 na 13,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 14, 2015

VPL 2015/2016:-Huu ndio msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara baada ya mechi za December 12 na 13,2015.

Ligi Kuu Vodacom, VPL, iliendelea Jumapili December 13,2015 ,kwa Mechi 2 na huko Tanga Mechi kali ya Dabi ya Jiji hilo kati ya Coastal Union na African Sports ilikwisha kwa Sare ya 1-1.

Kwenye Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam, JKT Ruvu iliichapa Tanzania Prisons 4-1.

Juzi Jumamosi, Jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Taifa, Azam FC na Simba zilitoka 2-2, huko Mkwakwani VPL-DES13Yanga kubanwa 0-0 na Mgambo JKT wakati Mbeya City ikitoka 2-2 na Mtibwa Sugar.

Matokeo hayo yameibakisha Azam FC kileleni ikiwa na Pointi 26, ikifuatiwa na Yanga yenye 24, Mtibwa Sugar 23 na Simba 22 huku Timu zote hizo zikiwa zimecheza Mechi 10.

LIGI KUU VODACOM 2015/2016.

Mechi zijazo

Jumatano Desemba 16,2015.

African Sports v Yanga

Jumamosi Desemba 19,2015.

Yanga v Stand United

Mwadui FC v Ndanda FC 

Kagera Sugar v African Sports

Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar

Toto Africans v Simba

Majimaji v Azam FC

Jumapili Desemba 20,2015.

JKT Ruvu v Coastal Union

Mbeya City v Mgambo JKT


 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad