CHALLENGE CUP 2015:-Ni Uganda Mabingwa mara 14 wakiifungwa Rwanda 1-0 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 05, 2015

CHALLENGE CUP 2015:-Ni Uganda Mabingwa mara 14 wakiifungwa Rwanda 1-0 .

Leo Desember 05,2015 huko Addis Ababa Nchini Ethiopia, Rwanda na Uganda zimecheza Fainali ya Kombe la Chalenji ambazo Mshindi wake hubeba Kombe linaloashiria ndio Nchi Bingwa ya Afrika Mashariki nay a Kati na pia kuzoa kitita cha Dola 30,000.

Timu itakayoibuka mshindi wa pili katika  Fainali hii itapewa Dola 20,000.

 Rwanda ilitinga Fainali hii baada ya kutoka 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo na Sudan na kushinda kwa Penati wakati Uganda pia ilikwenda Sare 0-0 na Wenyeji katika Dakika  Uganda ‘The Cranes’ wameibuka mabingwa wa michuano ya Chalenji iliyomalizika leo nchini Ethiopia.

Katika fainali hiyo-UGANDA wamefanikiwa kutwaa taji la 14 la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge CUP 2015 baada ya kuifunga Rwanda bao 1-0 jioni ya leo nchini Ethiopia katika mchezo wa fainali.

Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Ceasar Okhuti aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Dennis Okot kwa kumtungua Eric Ndayishimiye dakika ya 15.

Kocha Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic ambaye amewahi kuifundisha Rwanda alikuwa mwenye furaha na akasema Uganda imedhihirisha ubora wake katika ukanda wa CECAFA.

Safu ya ilinzi ya Uganda ilikuwa inaongozwa na beki wa Simba, Juuko Murishid ambaye ameingoza timu hiyo kubebwa ubingwa dhidi ya Rwanda ambayo ilikuwa na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzoma na kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza.

“NInafurahia kazi, ni furaha kubwa, tumedhihirisha sisi ni bora katika ukanda huu, tukiwa timu pekee iliyofuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 Urusi, na tunabeba Kombe la Challenge,”amesema.

Mapema katika mchezo uliotangulia, wenyeji Ethiopia walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Sudan kwa penalti 5- 4 kufuatia sare ya 1-1.
 
 
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
   

Post Bottom Ad