AJALI / PICHA:-Semi -trela laangukia Mtu na Kufariki Papo Hapo....Kagunga,wilyani Kasulu-Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 05, 2015

AJALI / PICHA:-Semi -trela laangukia Mtu na Kufariki Papo Hapo....Kagunga,wilyani Kasulu-Kigoma.

Mwanamke mmoja mkazi wa Kagunga wilayani Kasulu mkoani Kigoma alietajwa kwa jina la Bi. Annastazia Ndihagati anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 51 amefariki dunia papo hapo baada ya kuangukiwa na gari kubwa la mizigo.

Ajali hiyo iliyotokea Desember 03,2015 majira ya saa 10 Alasiri,baada ya gari la mizigo sem trela aina ya MAN lenye namba za usajiri T 817 BDK lililokuwa limekwama kwa kutitia katika eneo hilo la mtaa wa Kagunga kutokana na Mvua kunyesha ,kisha gari hilo kumuangukia Mama huyo kutokana na kuwa na mzigo mkubwa uliopakiwa katika gari hilo.
Gari hilo liliinuliwa baada ya mzigo kufaulisha na mwili wa marehemu ukapatikana majira ya saa 6 usiku ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kasulu limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na liliuchukua mwili huo na kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kasulu ya Mlimani kwa hatua zaidi.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

  

Post Bottom Ad