CECAFA CHALENJI CUP 2015:-Rwanda na Sudan zaenda Nusu fainali.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 01, 2015

CECAFA CHALENJI CUP 2015:-Rwanda na Sudan zaenda Nusu fainali.!

Hatua  ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Challenge 2015 iliendelea kwa timu ya taifa ya Rwanda kucheza mchezo wao na timu ya taifa ya Kenya, ikiwa ni siku moja toka Kilimanjaro Stars itolewe na mwenyeji wa mashindano hayo Ethiopia kwa mikwaju ya penati.
amavubi1_l643_h643
Leo ,Desember 01,2015,Mechi zote mbili za Robo Fainali za Mashindano ya CECAFA CHALENJI CUP 2015 ziliisha kwa Sare ya 0-0 katika Dakika 90 na Washindi kutinga Nusu Fainali kwa Mikwaju ya Penati 5-3.

Mapema, South Sudan na Sudan zilitoka 0-0 na Sudan kusonga kwa Penati 5-3 na kufuatiwa na Rwanda na Kenya pia kutoka 0-0 na Rwanda kusonga kwa Penati 5-3.

Katika Nusu Fainali, Ethiopia itakutana na Uganda wakati Rwanda ikicheza na Sudan kwenye Mechi zitakazochezwa Alhamisi.

RATIBA/MATOKEO.

Robo Fainali

Jumatatu Novemba 30,2015.

Uganda 2 – 0 Malawi

Kilimanjaro Stars 1 – 1 Ethiopia  [Ethiopia yasonga kwa Penati 4-3]

Jumanne Desemba 1,2015.

South Sudan 0 – 0 Sudan  [Sudan yasonga kwa Penati 5-3]

Rwanda 0 – 0 Kenya  [Rwanda yasonga kwa Penati 5-3]

Nusu Fainali.

Alhamisi Desemba 3,2015.

Uganda v Ethiopia

Sudan v Rwanda

Jumamosi Desemba 5,2015.

Mshindi wa Tatu

Uganda/Ethiopia v Sudan/Rwanda

Fainali.

Uganda/Ethiopia v Sudan/Rwanda

1407020336amavubi-players
Rwanda wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 5-3, mikwaju ya penati ya Haruna Niyonzima, Tuyisenge na Kizimana ilisaidia Rwanda kutinga hatua ya robo fainli ya michuano hiyo, kwa matokeo hayo sasa rasmi Kenya ambao walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo wamevuliwa ubingwa. 

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad