Waziri Mkuu
Mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim
Majaliwa ameshinda kwa kura za ndiyo 258 sawa na asilimia 73.5 ya kura zote
zilizopigwa na wabunge leo,November 19,2015 wakati kura za hapana zikiwa 91, sawa na asilimia
25.9.
Jina hilo lililoteuliwa na Rais Dk. Magufuli kushika
nafasi hiyo ni la Mbunge wa Ruangwa, Majaliwa Kassim Majaliwa ambaye alikuwa
Naibu Waziri wa TAMISEMI katika Serikali ya awamu ya Nne ya Rais Mstaafu Jakaya
Kikwete.
Bw Majaliwa,
55, amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa (kusini mashariki mwa Tanzania), Jimbo
la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010.
Bw Majaliwa,
ambaye ni mwalimu kitaaluma, atamrithi Bw Mizengo Pinda ambaye alihudumu kama
Waziri Mkuu chini ya Rais mstaafu Kikwete kuanzia 2008.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment