|
Treni hiyo
baada ya kupata ajali.
Watu wapatao
16 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye ajali ya treni
iliyotokea katika Wilaya ya Bolan, jimbo la Baluchistan, Kusini Magharibi mwa
Pakistani, jana,November 17,2015.
Mamlaka ya
Reli nchini Pakistani imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa,
ajali iliyotokea karibu na Mji wa Quetta, Makao Makuu ya jimbo la Baluchistan
baada ya breki zake kushindwa kufanya kazi wakati wa ikipandisha mlima hivyo
kupelekea kuanguka.
Treni hiyo
iliyokuwa na abiria takribani 300, baada ya ajali majeruhi walipelekwa
hospitali kwa ndege maalum ya uokoaji iliyowahi kufika eneo la tukio.
Waliokufakwenye
ajali hiyo ni abiria 12, dereva wa treni hiyo na msaidizi wake na Maofisa
Polisi wawili wa Mamlaka ya Reli.
Ajali
nyingine kama hiyo ilitokea nchini Pakstani Julai 17, mwaka huu iliyouwa watu
baada ya treni maalum ya mafunzo ya kijeshi ilipoanguka baada ya kuvunjika kwa
daraja.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment