![]() |
|
Kwa bahati
mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na
gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya
ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana
nyenzo za kumfanyia uchunguzi.
Katika
uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa
Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya
baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi
nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani
kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake
wote wawili kufariki dunia.
Hawezi kukaa
wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na
bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo
nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini ili kumsaidia Joyce
inatakiwa aanze mchakato (process) upya
za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
|

Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari
maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki
yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa
hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni
vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea
kupata tiba 500,000/-
Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi
3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu.
Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.
Deo Kakuru Msimu,Msamaria mwema
SIMU +255769
512 420
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
------------------------------ --------
UPDATES:
Wasamaria
wema kadhaa wamejitokeza kumsaidia dada Joyce. Hatuna uhakika kwamba wote
wanapenda majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji
wa Tshs:
1.
505,000/-
2.
50,000/-
3.100,270/-
4.
10,000/-
5.
100,000/-
6.
500,000/- (ahadi ya uhakika)
7.
500,000/- (Michuzi Media Group)
7.
800,000/- (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa
atapofikishwa Dar es salaam).
Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/- tayari zimekusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa.
Pamoja
na yote hayo, kiasi cha Tshs. 3,000,000/- za ziada zinahitajika kwa ajili ya
kuhitimisha zoezi lote hili. Hiyo ikiwa ni gharama za usafiri, malazi ya
mgongwa na wasaidizi wawili kwa mwezi mmoja (atapopelekwa Dar es salaam kwa
vipimo na matibabu) ili kumsaidia. Hivyo michango zaidi inahitajika kumuokoa
dada Joyce.
KUTOA NI MOYO.
Aidha,
kwa kiasi kilichopatikan, mipango imeshafanywa kumpeleka dada Joyce katika
hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa uchunguzi mpya wa awali. Baada ya hapo
tutawafahamisha nini kinachotakiwa kuendelea.
Deo
Kakuru Msimu
Msamaria
mwema
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea sio tu kuchangia bali pia kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .







No comments:
Post a Comment