VIPAJI VYETU:-Rwanda ni mabingwa wa 'Tour of Rwanda 2015.' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 23, 2015

VIPAJI VYETU:-Rwanda ni mabingwa wa 'Tour of Rwanda 2015.'


Kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa timu kutoka Eritrea. 

Timu ya waendeshaji baiskeli kutoka Rwanda ilinawiri katika mashindano ya kimataifa ya Tour of Rwanda 2015 yaliyomalizika mjini Kigali.

Timu ya Rwanda ilihifadhi ubingwa wa mashindano hayo Tour of Rwanda 2015.

Jean Bosco Nsengimana mwenye umri wa miaka 22 ameibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyozunguka Rwanda kwa wiki nzima yakishirikisha jumla ya waendesha baiskeli 60 kutoka kona zote duniani.

Nsengimana aliwashinda nguvu wenzie wa timu ya Rwanda Joseph Aleluya aliyemaliza katika nafasi ya pili na Camera Hakuzimana aliyechukua nafasi ya tatu.

Jean Bosco Nsengimana mwenye umri wa miaka 22 ameibuka mshindi wa mashindano ya Tour of Rwanda2015.

Pia gwiji wa mchezo huo Debesay Mekseb ,mwenye uraia wa Eritrea lakini akichezea timu ya Bike Aid ya Ujerumani , licha ya kushinda awamu 4 kati ya awamu 7 za mashindano hayo hakuweza kupangua dakika 3 ambazo wanyarwanda walimzidi.

Hii ni mara ya pili mfululizo waendesha baiskeli hao kutoka Rwanda kunyakua taji kuu katika mashindano hayo ya Tour of Rwanda yaliyoko kwenye kalenda ya mashindano ya mbio za baiskeli barani Afrika yanayotambuliwa na shirikisho la dunia la mbio za baiskeli.

Na:-BBC SWAHILI.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad