UWAJIBIKAJI:- Mkuu wa Wilaya ya Chato,Mkoani Geita aanza na Kilimo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 25, 2015

UWAJIBIKAJI:- Mkuu wa Wilaya ya Chato,Mkoani Geita aanza na Kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Chato,mkoani Geita, Bw. Shaaban Ntarambe amesema wataalamu wa kilimo vijijini wanao wajibu mkubwa katika kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara unaongezeka na kukidhi mahitaji ya jamii na masoko.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kilimo wilayani hapa ziara ambayo ameifanya kwenye tarafa zote tano ambapo ziara hiyo pia ilikuwa na lengo la kujitambulisha kwake tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Wilaya hiyo mwezi Oktoba, 2015 .

 Akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mkuu wa Wilaya amewaagiza wataalamu wote wa kilimo kutokukaa ofisini na badala yake watembelee wakulima na kuwashauri juu ya kilimo bora na kanuni zake, “Najua wengi wenu mpo likizo, mubadilike kwani vigezo vya kupendana katika kazi viwe katika misingi ya kazi wasaidieni wakulima” alisema Mkuu wa Wilaya.

Mbali na kusitiza juu ya kilimo cha Pamba Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza wataalamu hao kuhakikisha wanakuwa na mashamba ya mfano katika maeneo wanayosimamia ili iwe rahisi hata kwa wakulima kujifunza kupitia mashamba hayo. Mashamba ya mfano yaliyosisitizwa ni ya mazao yote ya msingi yanayolimwa wilayani hapa ambayo ni Mpunga, Alizeti, Mahindi na Mhogo.

Bw. Ntarambe amewaagiza maafisa ugani wote kuhakikisha wanapima mashamba ya wakulima wote waliopo wilayani Chato ili kuwa na takwimu sahihi za eneo lililolimwa msimu wa 2015/2016.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Bw. Shaaban Ntarambe (Pichani)

 Watendaji na maafisa ugani wa tarafa ya Buseresere wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya chato (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kuhamasisha kilimo.

Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza wataalamu wa kilimo wanawafundishe na kuhakikisha wakulima wote wanafuata kanuni za kilimo bora ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea na kupanda kwa nafasi na kusimamia usambazaji wa pembejeo za ruzuku na kuhakiksha walengwa wananufaika na mpango huo.
Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza wataalamu wa kilimo wanawafundishe na kuhakikisha wakulima wote wanafuata kanuni za kilimo bora ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea na kupanda kwa nafasi na kusimamia usambazaji wa pembejeo za ruzuku na kuhakiksha walengwa wananufaika na mpango huo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mhandisi Joel Hari amewataka watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya wahamiaji wanaohamia wilayani hapa ambapo amewataka kuwa na daftari maalumu la wahamiaji ili kuepuka kuwa na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani. 

 Amewataka watendaji na wataalamu wa ugani vijijini kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi zenye kuleta tija katika jamii.

Watendaji na maafisa ugani wa tarafa ya Chato wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya chato (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kuhamasisha kilimo.

Na Richard Bagolele- Chato.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad