UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016:-Zifahamu timu zilizofuzu 16 na Matokeo ya Mechi za Jana Novemver 25. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 26, 2015

UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016:-Zifahamu timu zilizofuzu 16 na Matokeo ya Mechi za Jana Novemver 25.

Hapo jana November 25, 2015, Mechi za 5 za Maundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016 zilizochezwa Usiku huko Ulaya, Juventus, Paris Saint Germaine, Benfica na Atletico Madrid zimefanikiwa kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zikiwa na Mechi 1 mkononi.

 Timu hizi zinaungana na Real Madrid, Manchester City na Zenit Sainta Petersburg, zilizofuzu mapema pamoja na FC Barcelona na Bayern Munich zilizotinga Raundi ya Mtoano Jumanne November 24,2015.


Na hapa chini ni matokeo ya mechi hizo , kwa Real Madrid wakiwa Ugenini huko Ukraine waliongoza 4-0 hadi Dakika ya 76 kwa Bao za Cristiano Ronaldo, Bao 2, Luka Modric na Carvajal lakini ndani ya Dakika 11 Shakhtar Donetsk wakapiga Bao 3 na gemu kwisha 4-3.

Ushindi huu wa 4-3 kwa Real umewafanya wamalize Kundi A wakiwa Washindi wa Kundi na kufuatiwa na PSG walioifunga Malmo 5-0 huko Sweden huku Zlatan Ibrahimovic akipiga Bao dhidi ya Timu yake ya Nyumbani kwao aliyochipukia nayo.

Huko Turin, Italy, Mario Mandzukic aliifungia Bao Juventus walipoifunga Manchester City 1-0 na kufuzu pamoja na Man City ambao walikuwa tayari wamefuzu kabla ya Mechi hii.


TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA MTOANO.

**Bado 7

Real Madrid

Paris St-Germain

Atletico Madrid

Benfica

Juventus 

Manchester City

Barcelona

Bayern Munich

Zenit St Petersburg

UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016.

Mechi za Mwisho za Makundi

RATIBA

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa

Jumanne Desemba 8,2015.

KUNDI A

Paris St Germain v Shakhtar Donetsk 
             
Real Madrid v Malmö FF 
            
KUNDI B

PSV v CSKA    
       
VfL Wolfsburg v Man United  
               
KUNDI C

Benfica v Atletico Madrid 
           
Galatasaray v FC Astana 
            
KUNDI D

Man City v Borussia Mönchengladbach    
        
Sevilla v Juventus   
          
Jumatano Desemba 9,2015.

KUNDI E

Bayer Leverkusen v Barcelona
               
Roma v BATE Borislov 
               
KUNDI F

Dinamo Zagreb v Bayern Munich  
         
Olympiakos v Arsenal   
              
KUNDI G

Chelsea v FC Porto    
       
Dynamo Kiev v Maccabi Tel Aviv  
          
KUNDI H

KAA Gent v Zenit Saint Petersburg  
               
Valencia v Lyon            

TAREHE MUHIMU.

Raundi za Mtoano.

-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14

**Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16

-Droo ya Robo Fainali: Machi 18

**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13

-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15

**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4

FAINALI

Mei 28,2016.

San Siro, Milan, Italy


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad