ZIARA YA AMANI AFRICA:-Tazama Picha Papa Francis awasili Kenya… ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 25, 2015

ZIARA YA AMANI AFRICA:-Tazama Picha Papa Francis awasili Kenya… ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita.

Papa Francis akisaini Kitabu cha Wageni ,hukuakitazamwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  mara tu alipowasili  nchini Kenya leo,November 25,2015,kwa ziara ya siku sita.

  Papa Francis akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kuwasili nchini humo ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita kwa nchi za Afrika za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati,  huku Papa akitarajiwa  kueneza ujumbe wake wa Amani, maridhiano, mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko. . Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta .

Ninaenda Kenya, Uganda na kwa ndugu zangu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati nikiwa na furaha,” shirika la habari la Reuters limemnukuu akisema.

Afisa wa mawasiliano wa Vatican Padri Federico Lombardi alisema kwamba kwa Jorge Mario Bergoglio, ambalo ndilo jina kamili la Papa Francis, hii itakuwa ziara yake ya kwanza kabisa Afrika.

Hii ni ziara ya 11 ya Francis akiwa kama papa nje ya Vatican. Mapapa wawili wamewahi kuzuru mataifa haya kabla yake.
  Papa Francis akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kuwasili nchini humo ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita kwa nchi za Afrika za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati,  . Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta na kulia ni Naibu Rais wa Kenya, William Ruto.

Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiangalia burudani ya ngoma ya utamaduni mara tu alipowasili uwanja wa ndege wa kimatiafa wa jomo Kinyetta nchini Kenya leo,November 25,2015….. Bofya hapa kusoma ratiba ya Papa Francis ziara yake Afrika.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad