UHALIFU:-Tazama Kobe 201 wakikamatwa uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere wakisafirishwa nje ya Nchi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 18, 2015

UHALIFU:-Tazama Kobe 201 wakikamatwa uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere wakisafirishwa nje ya Nchi.

Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs). 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia November 17,2015 na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. 

(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii).


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad