Kikosi cha
timua ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichofungwa mabao 7-0 usiku
wa Jana November 17,2015 na wenyeji Algeria mjini Blida katika mchezo wa kufuzu
Kombe la Dunia 2018,kinatarajiwa kuondoka leo November 18,2015 (Jumatano)
asubuhi na itafika Dar es Salaam Alfajiri ya Alhamisi.
Safari ya
nchi 20 zitakazoingia hatua ya Makundi
ya kuwania Nafasi 5 za Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018
huko Russia zimekamilika hiyo Jana baada ya Mechi za Marudiano za raundi ya
Pili huku Tanzania ikicharazwa 7-0 na Algeria na kutupwa nje.
Tanzania,
wakicheza ugenini, walidundwa 3-0 hadi Mapumziko na kwenda hiyo Haftaimu wakiwa
pungufu baada ya Mudathir kula Kadi Nyekundu katika Dakika ya 41 baada ya
kupewa Kadi za Njano 2 ya kwanza ikiwa katika Dakika ya 1 tu ya mchezo.
Tanzania,
ambayo ilitoka 2-2 na Algeria katika Mechi ya Kwanza, ilipewa Jumla ya Kadi za
Njano 7 na kufungwa kwa Penati 2 juu yake kwenye Mechi hii iliyochezeshwa na
Refa Sidi Alioum kutoka Cameroun.
Tanzania
sasa imetupwa nje ya safari ya kwenda Russia kwenye Fainali za Kombe la Dunia
zitakazochezwa Mwaka 2018 kwa kucharazwa Jumla ya Mabao 9-2 na hizi ni Bao
nyingi mno kufungwa kwake Miaka hii ya hivi karibuni.
NCHI 20
ZILIZOFUZU HATUA YA MAKUNDI.
-Gabon
-Zambia
-Uganda
-Congo DR
-Morocco
-Guinea
-Libya
-Cameroun
-Ghana
-Congo
-Nigeria
-Egypt
-Tunisia
-South
Africa
-Ivory Coast
-Burkina
Faso
-Algeria
-Cape Verde
-Senegal
**Timu hizi
20 zitapangwa Makundi Matano ya Timu 4 kila moja na Mshindi wa kila Kundi
kutinga kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment