|
Spika,Job Ndugai
akivaa joho rasmi na kuingia tena Bungeni akiongozwa na maaskari wa Bunge na
kisha kuapishwa na Katibu wa Bunge.
Mbunge
wa Kongwa mkoani Dodoma, Job Yustino Ndugai (55) ndiye Spika mpya wa Bunge
atakayeongoza Bunge la 11 lililoanza mkutano wake wa kwanza jana November
17,2015.
Ndugai,
ambaye ni Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alichaguliwa kwa kishindo,
akitwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea wengine saba kutoka vyama vya
siasa kwa kupata asilimia 70 ya kura zote zilizopigwa.
Ndugai
aliyekuwa Naibu Spika katika Bunge la 10, alipata kura 254 akifuatiwa na
mgombea wa Chadema, Goodluck Ole Medeye aliyepata kura 109, huku kura
zilizopigwa zilikuwa 365 na kura mbili ziliharibika.
Wagombea
wengine sita na vyama vyao katika mabano ambao hawakupata kura ni Peter Sarungi
(AFP), Hassan Almas (NRA), Dk Godfrey Malisa (CCK), Richard Lyimo (TLP), Hashim
Rungwe (Chaumma) na Robert Kasinini (DP).
Kutokana na
ushindi huo, Ndugai anakuwa Spika wa sita wa Bunge hilo akitanguliwa na Adam
Sapi Mkwawa kuanzia 1964 hadi Novemba 19, 1973, kisha aliingia Erasto Mang’enya
Novemba 20, 1973 hadi Novemba 5, 1975, kisha alirudi tena Mkwawa kuanzia
Novemba 6, 1975 hadi Aprili 25, 1994.
Wengine ni Pius Msekwa Aprili 28, 1994
hadi Novemba 20, 2005, Samuel Sitta Desemba 26, 2005 hadi Novemba 2010, kisha
Anne Makinda Novemba 12,2010 hadi November ,17,2015.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment