Tayari Nafasi
3 kati ya 16 za Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI 2015/2016,zimeshachukuliwa
na Klabu 3 na bado zipo Klabu 27 kati ya 29 zilizobaki kwenye Makundi zenye
nafasi za kuchukua Nafasi 13 zilizobaki.
KLABU
ZILIZOFUZU KUINGIA MTOANO.
-Real
Madrid
-Manchester
City
-Zenit
Saint Petersburg
IFUATAYO
NI HALI YA KILA KUNDI KWA MECHI ZA JUMANNE NA JUMATANO.
Jumanne
Novemba 24,2015.
KUNDI
E.
-Barcelona
(Pointi 10) v Roma (5)
-BATE
Borisov (3) v Bayer Leverkusen (4)
Barcelona watasonga
kama Washindi wa Kundi wakipata Sare na pia wanaweza kufuzu wakifungwa ikiwa
Leverkusen watashindwa kushinda.
Ikiwa BATE
na Leverkusen zitatoka Sare basi watupwa nje ya Timu mbili za juu ikiwa AS Roma
watashinda.
Ikiwa BATE
watafungwa na AS Roma kushinda, BATE watamaliza Nafasi ya 4.
KUNDI
F.
-Bayern
München (Pointi 9) v Olympiacos (9)
-Arsenal
(3) v Dinamo Zagreb (3)
Sare kwa
Bayern na Olympiacos itawatosha kutinga Raundi ya Mtoano.
Arsenal
wanahitaji kushinda na kuombea Olympiacos wafungwe ili wapate nafasi ya
kuifunga Olympiacos katika Mechi ya mwisho ya Kundi na wao kufuzu lakini
inabidi ushindi uwe bora kuliko Olympiacos walipoifunga Arsenal 3-2 katika
Mechi yao ya kwanza.
Arsenal
hawawezi kuipita Bayern.
KUNDI
G.
-Porto
(Pointi 10) v Dynamo Kyiv (5)
-Maccabi
Tel-Aviv (0) v Chelsea (7)
Porto
watafuzu kwa Sare.
Chelsea
watafuzu wakishinda na Dynamo kushindwa kupata ushindi.
KUNDI
H.
-Zenit
(Pointi 12, Washafuzu) v Valencia (6)
-Lyon
(1) v Gent (4)
Zenit
wameshafuzu na watatwaa Nafasi ya Kwanza ya Kundi wakishinda.
Valencia
watafuzu wakishinda huku Gent wasishinde.
Jumatano
Novemba 25,2015.
KUNDI
A.
-Malmö
(Pointi 3) v Paris Saint-Germain (7)
-Shakhtar
Donetsk (3) v Real Madrid (10, Washafuzu)
Real Madrid
wameshafuzu na watashinda Kundi hili wakiwa Namba 1 ikiwa watashinda au
wakitoka Sare ikiwa PSG haishindi n ahata wakifungwa wanaweza kuwa Namba 1
ikiwa PSG itafungwa.
PSG
watafuzu wakishinda au kwa Sare ikiwa Shakhtar haishindi.
KUNDI
B.
-CSKA
Moskva (Pointi 4) v Wolfsburg (6)
-Manchester
United (7) v PSV Eindhoven (6)
Man United
watafuzu wakishinda.
CSKA
hawatafuzu wakifungwa.
KUNDI
C.
-Astana
(Pointi 3) v Benfica (9)
-Atlético
Madrid (8) v Galatasaray (4)
Benfica
watasonga wakishinda na pia wakitoka Sare ikiwa Atletico itaifunga Galatasaray
au kwenda Sare.
Ikiwa
Benfica watashinda na Atletico hawashindi, basi Benfica watatwaa Nafasi ya
Kwanza.
Atlético
wanahitaji Sare kufuzu.
KUNDI
D.
-Juventus
(Pointi 8) v Manchester City (9, Washafuzu)
-Borussia
Mönchengladbach (2) v Sevilla (3)
Man City
wameshafuzu na watatwaa Nafasi ya Kwanza kwa ushindi.
Juventus
watafuzu wakishinda au wakipata matokeo yeyote yale ili mradi Sevilla
wasishinde.
Ili kuweka
hai matumaini ya kufuzu, Sevilla lazima waifunge Mönchengladbach na kungojea
Mechi ya mwisho na Juventus hapo Desemba 8 washinde ili wafuzu ingawa kwenye
Mechi hiyo wasipoifunga Juve basi wabahakika ya kwenda EUROPA LIGI ambako
walitwaa Ubingwa wake kwa Misimu Miwili iliyopita.
UEFA
CHAMPIONZ LIGI 2015/2016 - RATIBA
**Mechi
zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa.
Jumanne
Novemba 24,2015.
KUNDI
E
2000 BATE
Borislov v Bayer Leverkusen
Barcelona v
AS
Roma
KUNDI
F
Arsenal v
Dinamo Zagreb
Bayern
Munich v
Olympiakos
KUNDI
G
FC Porto v
Dynamo
Kiev
Maccabi Tel
Aviv v Chelsea
KUNDI
H
2000 Zenit
Saint Petersburg v
Valencia
Lyon v KAA
Gent
Jumatano
Novemba 25,2015.
KUNDI
A
Malmö FF v
Paris St
Germaine
Shakhtar
Donetsk v Real
Madrid
KUNDI
B
2000 CSKA v
VfL Wolfsburg
Man United
v PSV Eindhoven
KUNDI
C
1800 FC
Astana v
Benfica
Atletico
Madrid v
Galatasaray
KUNDI
D
Borussia
Mönchengladbach v
Sevilla
Juventus v
Man City
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment