![]() |
|
Mshindi
namba moja wa shindano la mwanaume mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe,
Mison Sere.
|
![]() |
|
Bingwa
mtetezi mara tatu wa shindano hilo ambaye kwa sasa ametwaa nafasi ya pili,
William Masvinu akiwa katika pozi.
|
![]() |
|
Washiriki
wote wa shindano hilo wakiwa jukwaa moja.
|
![]() |
|
Bingwa
mtetezi mara tatu wa shindano hilo, William Masvinu akifanya yake ili apewe
kura za ushindi.
|
![]() |
|
Mison Sere
akitabasamu wakati wa mashindano hayo.
|
![]() |
|
Baadhi ya
washiriki wa shindano hilo.
|
![]() |
|
Mison Sere
na mkewe wakifufahia.
Harare,
Zimbabwe
Mjini Harare
nchini Zimbabwe, hivi karibuni kumefanyika mashindano ya kipekee ya kumpigia
kura mwanaume mwenye sura mbaya zaidi katika taifa hilo, mashindano yaliyoitwa
‘MrUgly’.
Kama
mashindano mengine ya urembo, shindano hili pia lilivutia washiriki wengi. Jopo
la majaji lilikua na mengi ya kutahini kando na sura walitizama hulka na
kujitanua kwa washindani
Kihoja
kilizuka pale waamuzi walipomtaja Mison Sere, kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu
la mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe akimbwaga mpinzani wake ambaye
ni bingwa mtetezi wa tuzo hizo William Masvinu akiambulia nafasi ya pili.
Hata hivyo
mashabiki wa bingwa mtetezi huyo, Masvinu walilalamikia uamuzi huo wakidai kuwa
Mison Sere alikuwa na sura nzuri tu ‘handsome’ licha ya mwanya mkubwa na
tabasamu kama ya kibogoyo.
Licha ya
majibizano makali Sere mwenye umri wa miaka 42, alipewa tuzo hiyo na kuzawadiwa
pesa kiasi cha dola $500, sawa na shilingi 1,000,000 za Kitanzania.
Yeye na mke
wake walishangilia tuzo hilo jukwaani na kuwatonesha kidonda wafuasi wa
mpinzani wake waliowazomea na hata kuzua vurugu wakidai kapendelewa.
‘Walihoji
umauzi wa majaji wakisema kuwa hakuwa na sura mbaya ila alikuwa kang’oa meno
yake ya mbele ili atwae ushindi huo.’
”Hayo sio
maumbile ya kutisha, kukosa meno?
”Inakuwaje
wanampuuza bingwa wa zamani William Masvinu ambaye maumbile yake yanatisha
mno”, walisikika mashabiki wa Masvinu. Mwisho wa mjadala huo ulibakia vivyo
hivyo.
Bingwa mara
tatu wa tuzo za mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe William Masvinu
alikwenda nyumbani akiwa na mfadhaikom mkubwa baada ya kuikosa nafasi ya
kwanza.
‘Huyu bwana
hatishi kamwe, hebu tazama pua langu kubwa uso wangu mweusi na unavyotisha,
sikio langu ni kama la popo ni kubwa itakuwaje kuwa amenishinda?’
‘La
sikubaliani na uamuzi huu wa leo, nimeudhika sana.” Masvinu alisikika
akinung’unika.
|
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.












No comments:
Post a Comment