![]() |
|
Mmoja wa
viongozi wa CHADEMA akiwatuliza wafuasi wa chama hicho waliokusanyika kwenye
hoteli ya Gold Crest,Jijini Mwanza.
|
![]() |
|
Jaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Lameck Mlacha, ametupilia mbali mapingamizi
yaliyowekwa na RPC wa Mwanza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya kesi
iliyofunguliwa jana na familia ya Marehemu Alphonce mawazo kuomba tafsri ya
mahakama baada ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya
kuuaga mwili wa marehemu.
Katika
mapingamizi hayo, mwanasheria mkuu wa serikali
alidai kuwa mleta maombi ambae ni Baba mdogo wa Mawazo hana uhalali wa
kisheria wa kuleta maombi hayo mahakamani
kwa kuwa yeye si baba mzazi wa marehemu, na kuwa hajaleta hoja za
kubishaniwa kwenye maombi hayo.
Upande wa
utetezi unaoongozwa na mawakili John Mallya, James Millya na Paul Kipeja
ulijibu hoja hizo kuwa katika hatua hiyo masuala ya kubishaniwa hayana sababu
ya kuletwa kwa kuwa ni hatua ya awali sana.
Kuhusu
uhalali wa kisheria wa baba mdogo wa marehemu, majibu yalikuwa kwamba baba
mdogo kwa kuwa ndiye aliemlea Marehemu Mawazo, anayo mamlaka na uhalali wa
kisheria wa kuleta maombi hayo.
Mahakama
imekubaliana na hoja za mawakili wa mleta maombi na kuamua kuruhusu kesi ya
msingi kufunguliwa kama ilivyoombwa, na kutupilia mbali mapingamizi ya RPC na
Mwanasheria mkuu.
Upande wa
wapeleka maombi utawasilisha maombi ya kesi ya msingi leo hii mchana, kisha
utasubiri maelekezo ya Mahakama kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa lini kisha
uamuzi wa kesi hiyo.
Alphonce
Mawazo alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA
mkoani Geita kabla ya kuuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu
wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu,2015 katika kijiji cha Katoro wilayani Geita.
|
![]() |
|
Kundi la
wafuasi wa chama hicho wakifuatilia kwa karibu kesi hiyo.
|
![]() |
![]() |
|
Polisi
wakilinda usalama.
|










No comments:
Post a Comment