TAZAMA VIDEO:-Hafla Ya Kumuapisha Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Chamwino Dodoma-Leo November 20,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 20, 2015

TAZAMA VIDEO:-Hafla Ya Kumuapisha Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Chamwino Dodoma-Leo November 20,2015.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, leo hii November 20,2015, amemuapisha Mbunge wa Ruangwa, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mjini Dodoma.


Hafla ya Kumuapisha Mh. Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Msitaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Wabunge na wageni wengine.




SIMU.TV:  Hatimaye Mhe Kassim Majaliwa ala kiapo cha uaminifu na kuahidi kuhifadhi na kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .BOFYA HAPA KUTAZAMA HAFLA YA KUAPISHWA KWA WAZIRI MKUU.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad