MSAADA WAHITAJIKA :-Kwa Mapacha walioungana wilayani Ngara/Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 21, 2015

MSAADA WAHITAJIKA :-Kwa Mapacha walioungana wilayani Ngara/Kagera.

Hawa watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/2015  mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji cha Nyarurama, Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara,Mkoani Kagera akielekea hopitali ya misheni Rulenge.

 Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani, hapo njiani.

 Baada ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni. 

Msamaria  amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa.

Inaelezwa na ma daktari hapo, wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.

Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchaango kwake ili aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.

Baba Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana uwezo hata wa kufika Dar.   

Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.

Mungu awabariki.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad