Lori lenye
kontena ambalo halijafungwa vizuri likiwa barabarani.
Katika hali
isiyo ya kawaida, Lori lenye namba za usajili T 498 AHS lililokuwa limebeba
kontena katika barabara ya Kilwa, kuelekea barabara ya Bandari/Shimo la Udongo
ambalo lilikuwa halijafungwa vizuri na kuonekana kuyumba bila wahusika kuchukua
hatua yoyote hivyo linaweza kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa
barabara ikiwemo kupelekea ajali.
Mara kadhaa
zimekuwa zikiripotiwa ajali zinazotokana na malori yaliyobeba makontena
kuanguka na mengine kudondokea watu na kusababisha uhalibifu wa mali na wakati
mwingine vifo.
Je, kwa hali
hii kweli ajali za namna hii zitaisha nchini?
|
No comments:
Post a Comment