Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli la kutaka fedha
zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya Wabunge
wapya zipelekwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kununulia
vitanda na magodoro ya Wagonjwa wanaolala chini, limetekelezwa.
Katibu mkuu kiongozi Balozi
Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300
vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, baiskeli za kubebea
Wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika hospitali
ya taifa Muhimbili.
Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda
vyote vimefungwa Jumapili ya November 22 2015 na kisha Rais mwenyewe
atakwenda Hospitalini hapo Jumatatu ya November 23 2015 viwe vyote vimefungwa
tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokosa vitanda.
Wadau mbalimbali walichangia kiasi
cha shilingi milioni mia mbili ishirini na tano (225) kwa ajili ya
kugharamia hafla ya Wabunge baada ya uzinduzi wa bunge la kumi na moja Dodoma
lakini Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi
shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo
la uhaba wa vitanda.
Gerson
Msigwa
Kaimu Mkurugenzi
wa Mawasiliano IKULU,
Novemba 21,
2015.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment