SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA:- Kesho November 17,2015 atapigiwa kura …CCM ni Job Ndugai jina lake lapitishwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 16, 2015

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA:- Kesho November 17,2015 atapigiwa kura …CCM ni Job Ndugai jina lake lapitishwa.

Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari leo November 16,2015,nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.

Baada ya kikao cha pamoja leo Dodoma, kamati ya wabunge wote wamepitisha jina la Mbunge huyo  kuwania nafasi ya Uspika na kesho November 17,2015, atapigiwa kura na wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pichani ni Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.

Kama tulivyoona wagombea wawili , Tulia Ackson na Abdullah Mwinyi walijitoa, hivyo Job Ndugai amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi sifa zake,” alisema Nape.

Kingine  leo November 16,2015, kutoka Dodoma ni uteuzi wa Rais Dk. John Magufuli ambaye amemteua Dkt.Tulia Ackson Mwansasu kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina la Mwansasu ambaye alikuwa mwanasheria mkuu msaidizi ni miongoni mwa majina matatu yaliyopitishwa jana,November 15,2015 na kamati kuu ya CCM akiwemo Job Ndugai pamoja na Abdullah Mwinyikuwania nafsi ya kiti cha spika.

Katibu wa Bunge Dkt.Thomas Kashillilah amethibitisha uteuzi huo ambao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 66 (e) inampa Rais madaraka kuteua wabunge wasiozidi kumi.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad