![]() |
|
Yaya Toure
BBC imetaja
majina matano yatakayowania tuzo hiyo,huku miongoni mwa majina hayo matatu ni kutoka Ligi Kuu Uingereza.
Tuzo hiyo ilianzishwa mwaka 1992 na uhusisha
waandishi wa habari kuchagua kwa kupiga kura za wachezaji watakaoingia katika Kutangazwa na baada ya hapo watu
wengine hupewa fursa ya kuchagua yupi anastahili kuibuka mshindi.
|
![]() |
|
Sadio Mane.
Majina matano yaliotajwa
kuingia katika kipengele hicho ni Pamoja na , Pierre-Emerick Aubameyang kutokea Gabon ,
anacheza katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Andre Ayew kutokea
Ghana , anakipiga katika klabu ya Swansea, Yacine Brahimi wa FC Porto , anatokea Algeria, Sadio Mane wa Senegal, anachezea klabu ya Southampton
na Yaya Toure kutokea Ivory Coast ,akiichezea Manchester City.
|
![]() |
| Yacine Brahimi |
![]() |
| Andre Ayew |
![]() |
|
Pierre-Emerick
Aubameyang
Mshindi
ataamuliwa na mashabiki wa soka Afrika ambao watapewa fursa kupiga kura hadi
tarehe 30, Novemba.
Unaweza
kupiga kura Mtandaoni kwa kubofya hapa au kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa
nambari….+44 7786 20 20 08:
Tuma 1 kumpigia Pierre-Emerick Aubameyang
Tuma 2 kumpigia Andre Ayew
Tuma 3 kumpigia Yacine Brahimi
Tuma 4 kumpigia Sadio Mane
Tuma 5 kumpigia Yaya Toure
Mshindi
atatangazwa Siku ya Ijumaa tarehe 11 mwezi December,2015 wakati wa matangazo maalum kwenye
BBC World News na BBC World Service, wakati mitandao ya BBC Sport na BBC Africaikitoa pia matangazo. Kwa sheria na masharti bofya hapa.
Rekodi ya
tuzo hizo kuanzia mwaka 2000 hadi 2014.
2000 Patrick Mboma – Cameroon na
Cagliari/Parma (Italia)
2001 Samuel Kuffuor – Ghana na Bayern Munich
(Ujerumani)
2002 El Hadji Diouf – Senegal na Lens
(France)/Liverpool (Uingereza)
2003 Jay-Jay Okocha – Nigeria na Bolton
Wanderers (Uingereza)
2004 Jay-Jay Okocha – Nigeria na Bolton
Wanderers (Uingereza)
2005 Mohamed Barakat – Egypt na Al Ahly
(Misri)
2006 Michael Essien – Ghana na Chelsea
(Uingereza)
2007 Emmanuel Adebayor – Togo na Arsenal
(Uingereza)
2008 Mohamed Aboutrika – Egypt na Al Ahly
(Misri)
2009 Didier Drogba – Ivory Coast na Chelsea
(Uingereza)
2010 Asamoah Gyan – Ghana na Sunderland (Uingereza)
2011 Andre Ayew – Ghana na Marseille
(Ufaransa)
2012 Christopher Katongo – Zambia na Henan
Construction (China)
2013 Yaya Toure – Ivory Coast na Manchester
City (Uingereza)
2014 Yacine Brahimi – Algeria na Porto
(Ureno)
2015 ………………..??????????
|











No comments:
Post a Comment