Chama cha
Mapinduzi CCM baada ya kumtangaza Bw. Job Ndugai kuwa mgombea nafasi ya Uspika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo atakutana na mgombea aliyesimamishwa na Umoja wa Vyama vinavyounda
UKAWA.
Umoja huo wa
vyama vinavyounda UKAWA –CUF,CHADEMA,NCCR-MAGEUZI NA NLD,wao wamemsimamisha Bw.Goodluck
Ole Medeye kugombea nafasi ya Uspika na Bi. Magdalena Sakaya kwa nafasi ya
Naibu spika wa Bunge akitegewa kuleta ushindani mkali kwenye kinyang'anyiro
hicho dhidi ya Dr. Tulia Ackson Mwansasu wa CCM ambaye mara baada ya kujiengua
nafasi ya juu ya Uspika amechukuwa fomu upande wa Naibu spika Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Majina ya
watu 8 wanaowania nafasi ya uspika wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
yaliyopokelewa na katibu wa bunge Dr.Thomas Kashilila ni haya hapa.
-Peter
Sarungi (AFP)
-Hassan
Kisabiya (N.R.A)
-Dkt Godfrey
Malisa (CCK)
-Job Ndugai
(CCM)
- Goodluck
Ole Medeye (CHADEMA)
-Richard
Lymo (T.L.P)
-Hashimu
Rungwe (CHAUMA)
-Robert
Kisinini (DP)
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment