Ofisa Habari
wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud.
Watu watano
waliokuwa wakichimba madini ya Dhahabu katika mgodi wa Nyangarata uliopo Wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga wamepatikana wakiwa hai baada ya kufukiwa na vifusi kwenye
mashimo ya mgodi huo kwa siku 41,zilizopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,November 16,2015, Ofisa Habari
wa Wizara ya Nishati na Madini, Bi.Badra Masoud amesema kuwa wachimbaji hao
wanaodaiwa kuwa sita, walifukiwa na vifusi mnamo Oktoba 05, mwaka huu 2015 na
kuendelea kuishi kwenye mashimo hayo huku wakila magome ya miti na udongo baada
ya kuishiwa chakula walichokuwa nancho, hadi jana Novemba 15,2015 walipookolewa
umbali wa kilomita 10 ndani ardhini na watano kati yao kukutwa hai huku mwenzao
mmoja akidaiwa kufariki dunia.
Baada ya
kupatikana wakiwa hai, manusra hao walikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya
Kahama ambako wanaendelea kupata matibabu muhimu kutokana kukutwa wakiwa
wamedhoofika kiafya.
Bi.Badra
amewataja waliopatikana hai kuwa ni; Joseph Bulule, Chacha Wambura, Unyiwa
Aindo, Msafiri Gerald na Muhangwa Amos, Wakati aliyefariki akimtaja kwa jina la
Mussa Supana.
Aidha mganga
mfawidhi wa hospitali ya Kahama Dr.Joseph Ngowi amethibitisha kupokea wahanga
hao wakiwa hai huku mmoja wa mashuhuda aliyefanikisha watu hao kuokolewa
akisimulia jinsi alivyogudua uwepo wa watu chini ya ardhi.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment