|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta
John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini
Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015
kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo,
Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa
Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki
kigumu.
Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa
Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo
na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa
tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na
shughuli zao za kila siku.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii
kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka
Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa
baadaye.
Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November 17, 2015.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment