KOMBE LA DUNIA 2018:- Taifa Stars yashindwa kulinda ushindi na kuiruhusu Algeria Sare ya 2-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 14, 2015

KOMBE LA DUNIA 2018:- Taifa Stars yashindwa kulinda ushindi na kuiruhusu Algeria Sare ya 2-2.


Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo November 14,2015, imeeshindwa kuchomoza  na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya Taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi kwa ajili ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

 Mshambuliaji Elius Maguli alianza kuifungia Taifa Stars bao la kuongoza dakika ya 43 kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi

Goli hilo likaipeleka Taifa Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza.
Maguli 1

Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria.

Taifa  Stars ilicheza mpira wa kasi na kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 54 lililofungwa na Mbwana Samatta baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Algeria kisha kufunga goli kwa ustadi wa hali ya juu.

Dakika ya 71 kipindi cha pili, Slimani Islam alifunga goli la kwanza kabla ya kuisawazishia Algeria dakika ya 74 goli lililotokana na kutoelewana kwa safu ya ulinzi ya Taifa Stars na kutoa mwanya kwa Slimani kuisawazishia timu yake.
Maguli 4


Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria

MATOKEO MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA AFRIKA 2018.                                                 
Afrika-Raundi ya Pili

**Saa za Bongo

Jumatano Novemba 11,2015.

Mozambique 1 – 0 Gabon 

Sudan 0 – 1 Zambia 

Alhamisi Novemba 12,2015.

Burundi 2 – 3 DR Congo 

Namibia 0 – 1 Guinea 

Benin 2 – 1 Burkina Faso 

Togo 0 – 1 Uganda 

Morocco 2 – 0 Equatorial Guinea

Ijumaa Novemba 13,2015.

Madagascar 2 – 2 Senegal 

Comoros 0 Ghana 0

Kenya 1 – 0 Cape Verde 

Libya 1 – 0 Rwanda 

Angola 1 – 3 South Africa 

Niger 0 – 3 Cameroon 

Liberia 0 – 1 Ivory Coast 

Swaziland 0 - 0 Nigeria 

Mauritania 1 – 2 Tunisia 

Jumamosi Novemba 14,2015.

Ethiopia 3 - 4 Congo 

Tanzania 2 -2 Algeria 

Chad 1 – 0  Egypt

1700 Botswana v Mali

2000 Gabon v Mozambique 

Jumapili Novemba 15,2015.

16:00 Zambia v Sudan 
    
16:00 Uganda v Togo   
    
17:30 Congo, DR v Burundi  
      
18:00 Equatorial Guinea v Morocco 
      
21:00 Guinea v Namibia

Jumanne Novemba 17,2015.

16:30 Rwanda v Libya     
 
17:00 Cameroon v Niger   

17:30 Congo v Ethiopia    

18:00 Ghana v Comoros    

18:00 Nigeria v Swaziland   
      
19:30 Egypt v Chad 

20:00 Tunisia v Mauritania 

20:00 South Africa v Angola  
     
20:00 Ivory Coast v Liberia    
    
21:00 Burkina Faso v Benin  
      
21:15 Algeria v Tanzania   

22:00 Cape Verde v Kenya 

22:00 Senegal v Madagascar  
    
22:00 Mali v Botswana

 **Washindi kutinga hatua ya Makundi.


MAGULI 5
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad