Mechi hiyo
ambayo kwa Chelsea ilikuwa ya 13 ya Ligi Kuu Uingereza toka kuanza kwa msimu
huu, ikiwa ishacheza mechi 12 na kushinda 3, imefungwa 7 na kutoa sare mechi 2
haikuwa rahisi kupata matokeo licha ya kuwa ilikuwa katika uwanja wake wa
nyumbani wa Stamford Bridge London kwani walikosa nafasi kadhaa za kufunga.
|
Ndani ya The
Hawthorns, Arsenal walikwaa kisiki walipotunguliwa 2-1 na West Bromwich Albion
waliotoka nyuma na kushinda Mechi hii ambayo Cazorla alikosa Penati ambayo
ingewapa Sare.
Arsenal
walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya28 la Olivier Giroud na WBA
kusawazisha kwa Bao la Dakika ya 35 la Morrison na kisha kujifunga mwenyewe
kupitia Mikel Arteta katika Dakika ya 40 na kuwapa uongozi wa 2-1 WBA.
Arsenal
walipata Penati katika Dakika ya 82 baada ya Chris Brunt kumchezea Faulo Alexis
Sanchez lakini Santi Cazorla akapaisha.
|
No comments:
Post a Comment