![]() |
|
Hivyo, zifuatazo hapa ni kazi na
majukumu ya kila moja ya “Gland” na madhara yake isipofanya kazi inavyostahili.
1. Pineal Gland Hii imekaa ipo katikati ya ubongo wa mwanaadam. Inakiwango kikubwa cha kupokea damu Zaidi ya viungo vingine vyote vya “Glandular” mwilini.
Kazi
kubwa ya Pinea Gland ni kuchakachua hormone itwayo “Melatonin” ambayo
inawajibika kuhakikisha maendeleo ya hali ya kuwa “kiume” au “kike” mwilini mwa
binaadam; “Seratonin”, ambayo ni “Hormone” muhimu kwa maendeleo ya akili pia.
Pia, hii “Gland”, inakazi nyingine ambayo ni kuangalia madadiliko ya tabia ya mwili za kila siku kama vile mabadiliko ya jinsi unavyo lala usiku au pengine mchana. 2. Pituitary Gland
Hii imepewa jina na tasisi za
sayansi ya madawa kama” Master Gland”, katika ukweli wa kazi yake hii
nikama mnara wa usambazao mawasiliano kwenye ubongo, sehemu ijulikanayo kama”
Hypothalamus” ni kiungo ndani ya ubongo kinacho miliki mawasiliano ya
mishipa ya fahamu kati ya mfumo wa “Glandular “na jinsi mwili unavyo kuwa
katika hali ya huzuni, sikitiko au furaha.
Hii “Gland” pia humiliki hali ya
makuzi na kurekebisha joto mwili. Pungufu la au ongezeko la kazi yake,
husababisha makuzi yasio kawaida na kuwa kibonge au mbilikimo.
3. Thyroid & Parathyroid Gland
Imekaa shingoni,
na inamiliki mabadiliko ya chakula kilicho liwa mwilini
“Metabolism”, na kumiliki kima cha joto mwilini”Body heat”.
Hali
kadhalika makuzi na uchafu ndani ya mwili. Panapokuwa na kasoro ya udogo au
ukubwa wa miliki hii, matokeo yake ni kukasirisha mishipa ya fahamu mwilini na
kuwa hoi au kuchoka kila mara.
Calcium na phosphorus zinamilikiwa na hii Gland.
4. Thymus Gland
Ipo katika ya kifua, na huwa kubwa
mno utotoni na mtoto afikiapo barehe inapungua kuwa robo ya umbo lake. Hii ni
silaha ya kinga za mwili kwa mashambulizi ya magonjwa ya nje ndani ya
mwili. Ina miliki udumishaji ulinzi wa kupambana na magonjwa nayayo shambulia
mwili.
5. Adrenal Glands
Hii ipo juu kidogo ya mafigo, kazi
yake hasa ni kutoa nguvu na moto la hali ya juu na kuamua penye jambo la hatari
au tukio, hisia ya mwanaadam aidha uamua kukimbia au kupigana kijasili
kwa kupambana na tukio lolote.
6. Pancreas
ipo chini kidogo ya tumbo na kazi yake ni
kuyeyusha kemikali ijulikanoyo kama “Enzyme”.
Katika utumbo mdogo, inachanganya
“Insulin” hormone inayo punguza nguvu za sukari katika damu.
Endapo Pancreas inashindwa kumiliki vyema utengenezaji wa Insulin
mwilini, basi sukari ya damu huimalika Zaidi katika mwili na matokeo yake
ni Diabetes mellitus au ugonjwa wa kisukari.
Pia papo hapo, Insulin
nyingi nayo sio nzuri, husababisha kutetemeka na udhaifu mwilini.
7. Gonards
Uume au uuke, na kazi yake ni kumiliki kazi ya
ngono. Zina changanya Endrogen ambayo ni hormone ya jinsia ya
kiume, pia Estrogen kwa wanawake.
Hizi zote zinafanya kazi ya tabia ya
mwili wa kike na kiume kwa jinsia zilivyo tofautiana.
Maumbile ya mwili mzima wa mwanaadam , inamilikiwa na hizo Hormones.
Hapo
ndipo utakuta, kupitia mazoezi ya aina ya “ Yoga Asanas”, mwili unaweza
kumiliki na kusawazisha mzani wenye kima cha wastani katika
uchanganyaji wa hizo hormones mwilini.
Mafunzo ya mazoezi ya Yoga, yanadhihirisha wazi kutokana na masomo mbalimbali ya uchunguzi toka vyuo vikuu vingi maarufu nchini Marekani na kuandikwa kwa majarida mbali mbali yenye malengo ya kuielimisha jamii kuhusu afya na maumbile kupitia mazoezi ya Yogasanas. Imeandikwa na mwalimu wa Yoga, Rumadha Fundi kupitia majarida ya chuo alicho somea filosofia ya Yoga cha “College of Neo Humanist Studies”, Gullringen, Sweden na pia Tiljala, Culcutta, West Bengal, India ’87. Sensei Rumadha Fundi , Yoga & Karate Instructor.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Monday, November 23, 2015
MICHEZO YETU:-Zoezi la Yoga na Mfumo wa " Endocrine Glands".
Tags
# DONDOO
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment